Kutuhusu

logoPrecious present truth ni huduma la kanisa la waadventista wasabato; hivyo basi tuanamini ujumbe wa biblia pekee na kufuata mashauri kutoka kwenye roho ya unabii. Precious Present Truth imeundwa kutimiza kazi ya Mungu ya kuwaita watu kujua ukweli wa neno lake na kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu inayopatikana katika ufunuo 14:6-12.

Imani yetu

Tunaamini kwamba Mungu ametuita ili tuishi maisha sawasawa na viwango vya kweli, na sio viwango vyetu wenyewe au viwango vya ulimwengu huu. Tunafahamu bayana kwamba shetani, adui wa kweli, anajaribu kuzuia kazi hii kutumia njia zozote zile. Lengo lake ni kufanya watakatifu wake Mungu kuwa mawindo yake. Bwana na mwokozi wetu Yesu kristo, aliyemshinda shetani hapo zamani, ndiye hakikisho kwamba hatafanikiwa.

Precious Present Truth tunaamini kwamba kanisa la wadventista wasabato ndio waliopewa jukumu la kuwaasa watu wa ulimwengu, kuwashauri kwamba tumekaribia malango ya mbinguni. Huu ni mzigo mkubwa mabegani mwetu, lakini ni mzigo tunaoweza kuubeba kwa furaha.

Kupitia huduma yetu tunataka kuwafikia watu wa mataifa yaliyoko Africa, kuinua utukufu wa Mungu na kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu. Ili kumaliza kazi hii, tunahitaji kuwapa habari kwa njia ya vyombo vya kisasa na kupitia vitabu , DVDs, na video za internet zitawekwa tayari kwa lugha nyingi, hata lugha zile za makabila za watu wa bara la Afrika.

Katika siku za usoni, Precious Present Truth ikishirikiana na makanisa zetu itaanda semina katika miji mikuu ya mataifa mengi ya afrika. Wazungumzaji watakuwa washiriki walio na ujuzi na uelewa mkubwa katika Nyanja za matengenezo za kiafya na unabii, pia na wale watakaofundisha njia inayofaa wakristo kufuata katika ulimwengu unaozidi kuwa hatari kwa ukristo wa kweli.

 

Kisa chetu

Precious Present Truth ilianza mwaka wa 2011 na kikundi kidogo cha washiriki wa kanisa la waadventista wasabato waliona msimamo dhabiti na wanaoelewa uharaka wa kutumia muda huu mfupi kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu sawa na matukio yanayotukio sasa na kuweka wazi hila za kisasa ili watu wajue tofauti kati ya kweli na uongo.

error: Content is protected !!