Ellen G. white

Ellen G white

Ellen G White

Kwa kifupi ellen white alikuwa mwanamke aliyekuwa na karama ya unabii aliyeishi katika karne ya 19 (1827-1915), lakini kwa kupitia maandiko yake anazidi kuathiri mamilioni ya watu ulimwenguni. Alipokuwa hai aliandika nyaraka, makala na vitabu 40, kwa sasa anazo kurasa 50000 za maandishi yake ukijumuisha zile zilizo wekwa pamoja na watu wengine..

Yeye ndiye mwandishi mwanamke aliyetafsiriwa sana katika historia ya fasihi, na ndiye mwandishi mwamerika aliyetafsiriwa sana kwa jinsia zote mbili. Maandishi yake yanajumuisha masomo mengi katika dini, elimu, mahusiano ya kijamii, uinjilisti, unabii, uchapishaji, lishe, na usimamizi.

Kazi yake kuu kwa maisha ya kikristo ni kitabu kiitwacho Njia Salama,ambacho imechapishwa katika lugha zaidi ya 140. Wadventista wasabato wanaamini kuwa Ellen white alikuwa na kipaji cha uandishi, wanaamini pia kuwa aliteuliwa na Mungu kama mjumbe maalum kurudisha umakini wa dunia katika biblia na kuwatayarisha watu kwa kurudi mara ya pili kwa kristo. Kutoka wakati alipokuwa na miaka 17 hadi alipokufa miaka 70 baadaye, Mungu alimpa takriban maono na ndoto 2000. Maono hayo yalitofautiana kwa urefu wa muda kutoka chini ya dakika hadi karibu masaa manne. Maarifa na mashauri aliyoyapokea aliyaandika ili yaweze kusambazwa kwa wengine. Ndiposa maandishi yake maalum yanakubalika na waadventista wasabato kama yaliyovuviwa, na ubora wake unatambuliwa hata kwa wasomaji wa kawaida.

Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha imani ya waadventista wasabato.. “ maandiko ya Ellen white sio mbadala kwa maandiko. Hayawezi kuwekwa katika kiwango sawa. Maandiko matakatifu yanajisimamia, kiwango maalum ambayo maandiko yake na maandishi yote yale lazima yalinganishwe ” ( imani ya wadventista wasabato…. Kamati ya huduma, kamati kuu ya wadventista wasabato Washington DC 1988, uk.227) hata hivyo Ellen White alibainisha “ licha ya kwamba Mungu amedhihirisha mapenzi yake kwa wanadamu kupitia neno lake , hajapunguza nguvu za uwepo wa roho mtakatifu aongozaye. Kinyume ni kwamba roho aliyeahidiwa na mwokozi wetu kulifunua neno kwa watumishi wake, kuangaza na kutusaidia kufuata mafundisho yake” (Pambano Kuu uk 7). Yafuatayo ni maelezo ya kina kuhusu maisha na kazi ya mwanamke huyu wa ajabu, akikidhi vipimo vyote vya nabii wa kweli kama jinsi yalivyowekwa katika maandiko matakatifu, naye alisaidia sana kuanzishwa kwa kanisa la wadventista wasabato.

Vitabu vya Ellen G white

error: Content is protected !!