Sisi ni nani?
“
Tunaomba kwamba Ujumbe wa Malaika Watatu uende ulimwenguni kote, ili tuweze kurudi nyumbani hivi karibuni.
”
UZALISHAJI
1. Zilizotafsiriwa kutoka katika lugha ya Kiingereza
PPT inatumia studio zake zilizopo Rwanda na Congo (DRC) kutafsiri, na kurekodi sauti (audio), mahubiri ambayo yamekwisha kurekodiwa ni ya hawa wafuatao;
- Professor Walter J. Veith
- Ivor Myers
- Doug Batchelor
- President Ted C. Wilson
- David Asscherick
- • Na wengine wanaopenda kushiriki Jumbe za malaika watatu
Masomo haya kwa njia ya video yanapatikana katika lugha za Kinyarwanda, Kifaransa, Kiswahili, Kilingala na Kitshiluba PPT inaeneza jumbe hizi kwa kukodi masaa kutoka katika vituo vya televisheni binafsi ambapo tunarusha ujumbe katika nchi ambazo zinazungumza lugha zilizotafsiri masomo hayo, pia tunahakikisha masomo haya yanapatikana katika chaneli zetu za Youtube na mitandao ya kijamii. Kwa sasa katika chaneli zetu za youtube tuna wafuatiliaji Zaidi ya 3,000 kila mwezi.
2. Zilizotafsiriwa Na Kuchapishwa Kwa Ajili Ya Kusambazwa
Kwa kushirikiana na Union ya Congo Magharibi, tumetafsiri vitabu kutoka katika lugha ya kiingereza kwenda katika Kinyarwanda, Kiswahili, na Kifaransa na vitabu vifuatavyo vilichapwa na kusambazwa;
- • Ukweli Usemwe – Profesa Walter J. Veith
- • Mpango Makini– Ivor Myers
- • Njia salama– Ellen G. White
- • Wazee na Manabii– Ellen G. White
- • Manabii na Wafalme- Ellen White
- • Majaribu hadi Ushindi– Ellen G. White
Vitabu vingine vingi katika lugha ya Kilingala, Kiswahili na Kitshiluba vinaendelea kutafsiriwa. Tunashirikiana na Konferensi za Afrika kusambaza vitabu hivi kupitia huduma mahalia za uchapishaji.
3. Mahubiri Katika Lugha Za Kiafrika
PPT imeshirikiana na wahubiri mbalimbali kutokea Afrika wanaorekodi jumbe na kuzisambaza kupitia televisheni binafsi zilizopo Afrika. Na matokeo yake maelfu ya watu wameendelea kubatizwa na kujiunga na makanisa ya Kiadventista, hususani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
PPT imerekodi na inaendelea kurekodi vitabu vya Ellen White kwa sauti katika lugha ya Kinyarwanda, Kiswahili, Kilingala, Kitshiluba na baadhi ya vitabu vilivyorekodiwa ni hivi;
. • Wazee na Manabii
. • Manabii na wafalme
. • Tumaini la Vizazi Vyote
. • Majaribu hadi Ushindi
. • Pambano Kuu
. • Elimu ya Kikristo
. • Matukio ya siku za Mwisho
. • Mashauri juu ya chakula
. • Huduma ya Uponyaji na vingine vingi.
PPT ina chaneli za Youtube kwa kila lugha zenye na wafuatiliaji Zaidi ya 3,000 kila mwezi.
4. Programu (Aplikesheni) ya Precious Present Truth
PPT imeanzisha programu (aplikesheni) inayoitwa “Precious Present Truth” unayoweza kuipakua bure katika simu janja za Android. Katika program hii unaweza kupata vitabu vya Ellen White kwa njia ya sauti na mahubiri mengine mengi katika lugha sita.
MIKUTANO YA HADHARA
Tunapanga kuwaalika wahubiri wazuri wa Kiadventista kutoka katika maeneo mbalimbali duniani waje kuhubiri barani Afrika, na wakati huo huo timu yetu ya mawasiliano itakuwa ikizirekodi jumbe hizi ili zirushwe katika televisheni na mitandao yetu ya kijamii.
Mungu ametubariki sana katika kazi hii kwa kuwaongoza wengi kwake, hatuna shaka kwamba ataifanikisha kwa kiasi kikubwa kuzidi tulivyofikiria.
MATOKEO
Kisa cha hivi karibuni: Watu wa Tshela, mji ulioko katikati ya Congo DRC, wamekuwa wakifuatilia jumbe hizi za malaika watatu kupitia televisheni ya Digital Congo, ambayo ni televisheni maarufu sana Congo. Neno la Mungu lilienea katika mji wote, kadri mmoja alivyomwambia mwenzake, wote wakawa na habari juu ya mahubiri haya kupitia televisheni hii. Matokeo yake, wote walishawishika na kusadikishwa kwamba wanapaswa kupumzika katika siku ya Sabato, wote walikuja kwa pamoja katika ofisi ya union ya Congo Magharibi wakiomba kujua maeneo ya karibu ambayo wanaweza kulipata kanisa la Waadventista Wasabato. Viongozi wa Union waligundua kwamba hakukuwa na kanisa huko Tshela, na kwa haraka kanisa liliwatuma walimu wa Biblia ili kuwasaidia hawa Waadventista wapya. Baada ya kufika pale, wazazi waliokuwa na watoto waliwauliza walimu hao wa biblia- Tumeshawishika kwamba tunapaswa kupumzika katika siku ya Sabato, lakini watoto wetu wanahudhuria shuleni katika siku ya Sabato, na sasa tunajua kwamba nao wanapaswa kupumzika siku ya Sabato, inawezekanaje ili nao wapumzike katika siku ya Sabato? Walimu wa Biblia waliwaomba wazazi wawajulishe idadi ya watoto hao ambao walihitaji kupumzika katika siku ya Sabato. Siku chache baadaye, wazazi walikuwa na idadi ya kustaajabisha ya wanafunzi 450. Kanisa lilifanya mpango wa kuwatafutia eneo la kufanyia ibada kila Sabato na wakaanzisha shule mpya ya Sabato katika eneo hilo kwa ajili ya watoto. Ijapokuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu, kwa sababu hawana madarasa mazuri, lakini wanamshukuru Mungu na kumheshimu katika Sabato yake.